Saidi Mrisho (aliyevaa nguo nyekundu) akituliza vurugu hizo.
FAINALI za michuano ya michezo soka kwa ajili ya Mei Mosi zilizomalizika juzi mkoani hapa ziliingia dosari baada ya timu za soka za Wizara ya Ulinzi na kiwanda cha kusindika Tumbaku cha mkoani hapa kuchapana makonde.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, ulikuwa ni katika kuadhimisha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani ambazo kitaifa zilifanyika mkoani hapa.
Vurugu hizo zilianza baada ya kumalizika kwa mchezo huo Wizara ya Ulinzi ikiwa imeibuka mshindi dhidi ya Tumbaku kwa magoli 2 – 1 ambapo mchezaji mmoja wa Tumbaku alidaiwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Ulinzi.
Timu ya Ulinzi ilikuwa imesheheni wachezaji wengi wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom kutoka Ruvu Shooting na JKT Ruvu, wakati Tumbaku ndiyo mabingwa wa ligi ya daraja la tatu mkoani Morogoro.
Katika vurumai hizo kocha mkuu wa timu ya Tumbaku, Saidi Mrisho au 'Zico wa Kilosa' ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, alifanikiwa kutuliza ghasia hizo akisaidiana na kocha msaidizi wa Ulinzi.
Monday, May 2, 2011
FAINALI SOKA MEI MOSI YASHUHUDIA MAKONDE MORO
Kocha msaidizi wa Ulinzi akimwondoa mshika bendera eneo la ghasia.
Labels:
www.mateja20.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment