Social Icons

Monday, April 11, 2011

UZINDUZI WA VIDEO YA MIRIAM WAFANA DAR

Miriam Lukindo akiimba wimbo wake wa ‘Ni Asubuhi’.
UZINDUZI wa albamu ya video ya ‘Ni Asubuhi’ ya mwanamuziki nyota wa Injili, Miriam Lukindo, akishirikiana na Haak Neel Production, uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam wikiendi hii, ulifana kwa hali ya juu baada ya kuvutia mamia ya mashabiki.
Uzinduzi huo uliowakutanisha waimbaji maarufu wa Injili wakiwemo Upendo Nkone, Maron Shako kutoka Kenya na Martha Mwaipaja na kwaya mbalimbali maarufu nchini, uliwafanya watu waliohudhuria katika hafla hiyo kuacha viti vyao na kujikuta wakiimba na kuserebuka kwa pamoja na waimbaji hao.

Miriam (kushoto) akimpa kipaza sauti Maron Shako ili aimbe wimbo wake wa ‘Nafsi Yangu’.


Maron akiimbia kwa hisia kali.


Miriam na Maron wakiimba kwa pamoja.


Shabiki (kulia) akiungana na Miriam jukwaani.


Wasanii wa filamu ambao ni mtu na mama yake, Susan Lewis ‘Natasha’ (kushoto) na mwanaye Yvonne Cheri (Monalisa) wakiserebuka na midundo ya Injili.


Miriam (katikati) akijimwaya na mashabiki wake.


Upendo Nkone akionyesha kipaji chake mbele ya kadamnasi.

0 comments: