Social Icons

Monday, April 11, 2011

A-Z AJALI YA EXTRA BONGO



Ajali hiyo ilitokea Jumamosi alfajiri maeneo ya Magomeni Mapipa katika Makutano ya Barabara ya Morogoro na Kawawa na kusababisha wasanii tisa kujeruhiwa.

Akianika A-Z ya tukio hilo, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ ambaye ndiye mkurugenzi wa bendi hiyo alisema kuwa, balaa hilo lilitokea wakati wasanii hao wakirejeshwa majumbani kwao baada ya kumalizika kwa shoo waliyokuwa wakiifanya ndani ya Ukumbi wa Meeda, Sinza Mori, Dar.

“Ilikuwa ni ajali mbaya sana, wasanii walikuwa ndani ya gari aina ya Nissan Civilian lenye namba za usajili T 850 BJS wakielekea Mwananyamala. Walikuwa wanarudishwa nyumbani baada ya kumaliza shoo pale Meeda Club.

“Walipofika Magomeni wakati wanataka kuvuka mataa, ghafla lilitokea gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba matenga ya nyanya na kuwagonga ubavuni.

“Yaani ni Mungu tu kwa kweli kwa sababu hakuna aliyefariki licha ya wasanii wapatao tisa kujeruhiwa vibaya,” alisema Choki.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Athanas Mwatanabo, Stamili Hamis, Gegori Steven, Mwantumu Athuman, Mwendambali Pablo, Jumanne Ally, Saidi Ramadhani, Abdallah King’ondo na Mfaume Zablon ambao walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.

Mateja 20 inawapa pole wasanii hao na linawaombea kwa Mungu wapone haraka ili waweze kurejea katika jukumu lao la kuiburudisha jamii.

0 comments: