Social Icons

Friday, April 22, 2011

Q- CHILLA ASAKWA NA POLISI



Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Aboubakar Katwila ‘Q Chilla’ anasakwa na polisi wa Kituo cha Oysterbay akidaiwa kufanya fujo katika Ukumbi wa Maisha Club uliopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Chanzo chetu cha habari kimetutonya kuwa, Q- Chilla alifanya tukio hilo usiku wa Aprili 17, mwaka huu ambapo anadaiwa kumfanyia vurugu meneja wa klabu hiyo aliyefahamika kwa jina la Sam Odera.

Ilidaiwa kuwa, awali msanii huyo akiwa ameongozana na washikaji zake wanne alifika ukumbini hapo na kutaka kuingia bila kufuata utaratibu, hali iliyosababisha kuzinguana na walinzi.

“Jamaa alikuwa anataka kuingia ukumbini pale kisanii, alipotakiwa kutulia na kufuata taratibu akaanza kuporomosha matusi.

“Kimsingi walifanya vurugu ya kufa mtu, wateja wakawa wanakimbia ovyo ndipo mmoja wa walinzi alikwenda polisi na kufungua jalada la kesi lenye namba OB/RB/6724/2011 KUFANYA VURUGU,”alidai mtoa habari huyo.

Baada ya kuzipata tetesi hizo, mwandishi wetu alimtafuta meneja wa klabu hiyo bila mafanikio lakini alipotafutwa mmoja wa maafisa usalama aliyefahamika kwa jina la Gidion Mashauri alisema:

“Mimi siyo msemaji wa Maisha Club lakini ni kweli tukio hilo lilitokea na tumeshalifikisha katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay.”

0 comments: