Social Icons

Friday, April 22, 2011

MISS DAR CITY CENTRE YAPAMBA MOTO

Wanakamati wa shindano hilo (mbele), wakiwa kwenye picha ya pamoja na warembo hao.
Wanakamati wa shindano hilo, wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkurugenzi wa Fetty Entertainments, Fatuma Abdallah 'Fetty' (aliyesimama nyuma kulia), wa kwanza kushoto ni Mwalimu wa warembo hao.
Mwalimu wa warembo hao Angel Ngakuka, akiwa kwenye pozi ndani ya Bustani za Lamada Hotel Ilala jijini Dar es Salaam wanakofanyia mazoezi warembo hao.
Mratibu wa shindano hilo Fetty, katika pozi
Warembo katika pozi

Mratibu wa shindano hilo Fatma Abdalah ‘Fetty’(mbele), akiwa kwenye pozi la pamoja na washiriki hao.

SHINDANO la kumasaka mrembo wa kitongoji cha Miss Dar City Centre 2011, linazidi kupamba moto kutokana na purukushani za mazoezi yanayoendelea katika kambi yao iliyopo Lamada Hotel Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao huu jana, mratibu wa shindano hilo, Fatma Abdalah ‘Fetty’, alisema kwamba kila kukicha anazidi kuridhizishwa na uwezo wa mazoezi ya warembo wake, na kwamba matumaini ya kutoa Miss Tanzania kwa kitongoji chake ni makubwa.

“Kiukweli ninazidi kuridhishwa na uwezo wa warembo wangu kila kukicha, na kufuatia uzuri walio nao natumaini mwaka huu naweza kutoa Miss Tanzania katika kitongoji change.”

Fetty, aliongeza kuwa hadi kwenye baadhi ya vitongoji alivyozungukia hajaona mrembo mwenye sifa za kuwazidi warembo wake.

“Kusema kweli tangu nimeanza kuzungukia kambi na mazoezi ya waandaaji wenzangu sijaona mrembo yeyote mwenye sifa za kuwazidi waembo wangu,” alisema Fetty.

Warembo wakijifua na mazoezi ndani ya ukumbi wa Lamada Hotel jana.


‘Rais wa Manzese’, Hamad Ally ‘Madee’ (katikati), akiwa kwenye pozi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo.

0 comments: