Social Icons

Friday, April 22, 2011

SIRI YAFICHUKA KUHUSU PENZI LA WEMA WALIOMPITAI SASA MAJUTO


Nyuma ya kasumba ya mastaa kupanga foleni kwa ajili ya penzi la Miss Tanzania ‘the history’ 2006/07, Wema Abraham Sepetu, ( pichani) kuna siri nzito ambayo imefichuka.

Uchunguzi wa gazeti bora la burudani Bongo, Ijumaa umebaini kuwepo kwa mastaa wanaommendea Wema ili kulamba maujiko na kujiweka juu kisanaa kwa kutumia jina la mrembo huyo anayetingisha vilivyo kwenye filamu za Kibongo kwa sasa.

Ripoti ya uchunguzi huo wa kipindi kirefu iliweka wazi kwamba, mara tu jamaa hao wanapopata ‘chansi’ ya kuwa na Wema, majina yao hupanda ghafla na inapotokea penzi kuyeyuka, baadhi yao hujikuta wakipoteza umaarufu.
“Wema amekuwa akitumiwa na hawa jamaa kwa kigezo cha mapenzi ili kukuza majina yao bila yeye kujua.

“Amekuwa akifanywa daraja la watu wanaotaka ustaa kwa kufanya jitihada za kuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi,” alifunguka msanii mmoja wa filamu kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini na kuongeza:
“Utakuta msanii hana jina kubwa ‘kiivo’ lakini akifanikiwa kuingia kwenye ‘malavidavi’ na Wema, anakuwa gumzo kutokana na vimbwanga vya mwanadada huyo.
WAACHWA NA MAJUTO

“Ni lazima washikaji wenye mawazo ya aina hiyo wajue kuwa Wema siyo mtu wa kudumu na mwanaume kwa muda mrefu ndiyo maana humwagana nao ‘fasta’ na kuwaacha na majuto ya kukosa penzi lake.
Baadhi ya mastaa waliowahi kutajwa kuwa na uhusiano na Wema bila kujulikana kama walikuwa na lengo la kujitwisha ustaa kupitia jina la mrembo huyo ni pamoja na mastaa wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’ na Herry Samir ‘Blu’.

Wengine ni staa wa filamu, Steven Kanumba, mjasiriamali Yusuf Jumbe, mkurugenzi wa Hartmann Productions, Hartmann Mbilinyi, mwimbaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel Mbwana ‘Chalz Baba’ na sasa yuko na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam juzi, Wema alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa ndiyo ‘sosi’ ya kumwagana nao mara tu anapogundua kwamba wana maslahi binafsi kwenye penzi lake.

AANZA NA MR CHUZ
Wema alilidadavulia Ijumaa kuwa, alianza kusikia ishu hiyo ya kufanywa daraja kutokana na jina lake alipokuwa akipiga mzigo kwa Mr Chuz.
Alisema: “Kwa mfano wakati niko kwa Chuz nilisikia watu wakisema kuwa jamaa alikuwa akilenga kuniweka kwenye himaya yake na wengine wakidai kuwa alikuwa mpenzi wangu, ukweli ni kwamba nilikuwa pale kikazi zaidi.”

KUHUSU HARTMANN
Wema alifunguka: “Kiukweli pale kwa Hartmann hakukuwa na kitu kingine zaidi ya kazi lakini nilishangaa watu walipoanza kutuchimba, niliwapotezea pamoja na kuwepo kwa ukweli kwamba jamaa alitaka kujaribu bahati yake akashindwa.”

JUMBE VIPI?

Mlimbwende huyo aliweka kila kitu hadharani kuhusu jamaa huyo: “Ni kweli Jumbe hakuwa maarufu lakini ndani ya kipindi kifupi akawa juu kwa sababu yangu. Baada ya kuachana naye, nasikia yuko kwenye filamu lakini hasikiki kabisa.”

CHALZ BABA APATA JINA ZAIDI
Akimzungumzia Chalz Baba, Wema alikoleza: “Pale Twanga Pepeta kuna wanamuziki wengi lakini nilipokuwa na Chalz Baba alipata jina zaidi kuliko wengine, unajua alipokuwa na mimi, mashabiki walipenda sana kumfuatilia. Baada ya kutengana nadhani ni mara chache sana anasikika.”

AKAFUNGA KAZI KWA DIAMOND
Mrembo huyo alidai kuwa, anaamini kuwa Diamond alimpenda kwa dhati na wanapendana sana: “Siamini kama ana maslahi binafsi, kwanza tumekutana tayari akiwa ni staa, nina imani tutadumu milele.”

Wema alimalizia kwa kukiri kuwa inawezekana amekuwa akitumika kama daraja la watu kujipatia ustaa lakini alisema kwamba ni fahari kwake kwa sababu ameweza kutengeneza watu wa kawaida wakawa mastaa.

0 comments: