Social Icons

Tuesday, April 12, 2011

MISS KILIMANJARO 2011 YAJA



SHINDANO la kumsaka Mlimbwende wa mkoa wa kilimanjaro 2011 linatalajiwa kuanza hivi karibuni baada ya waandaji wa shindano hilo kudai kuwa sehemu kubwa ya maandalizi yao imeshakamilika.

Akizungumza na Mateja20, mmoja wa waratibu wa sindano hilo Methuselah Magese, aliesema kuwa yeye na muandaji mwenzake wa shindano hilo, Jaquekline chuwa, mchakato umeanza na kwamba lazima miss Tanzania mwaka huu atatokea mkoa wa Kilimanjaro.
Shindano hilo litafanyika juni 11 ndani ya hoteli ya Salsanero, iliyopo maeneo ya shant town mjini moshi.

Magese aliongeza kwamba shughuli ya kumatafuta mlimbwende huyo itasimamiwa na Masanja Mkandamizajiwa kundi la Olijino Komedi akiwa kama mc wa shughuli hiyo.


Alisema kwa upande wa burudani kutakuwa na 20%, ambaye tayali wameshaafikiana kufanya nae kazi siku hiyo, na hapo badae wasanii wengine watatajwa watakao kuwepo kwenye mchakato huo.


Miss kilimanjaro 2011, imedhaminiwa na Vodacom,redds,Africa sana pub,rafiki min super market,Excutive solution,Bamm solution na blog ya uniqueentertz.
"Tunawaomba warembo wanaojiamini kuwa wao ni warembo na wenye ari ya kuwa vinara wa sanaa ya urembo wajitokeze kuwania taji hilo ambalo litakuwa na ushabiki wa aina yake kwani tunategemea kutoa warembo bomba ambao watatoa changamoto kwa vitongoji na kanda zingine" alisema Magese.

0 comments: