Social Icons

Wednesday, April 13, 2011

AFARIKI BAADA YA KUJERUIWA ALIPOKUA ANASHUSHA VIOO KWENYE GARI



KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Shabani Dede jana mchana alijeruhiwa vibaya baada ya kutumbukia kwenye boksi la vioo alilokuwa akilishusha kwenye lori aina ya Isuzu namba za usajiri T603 AGG ili kuviingiza kwenye duka la mfanyabiasha mwenye asili ya Kiasia, Mtaa wa Mlapakolo, jirani na Hotel ya Mount Uluguru ambapo alifunikwa na vioo hivyo na vingine vikimkata sehemu mbali mbali za mwili wake.

Mtandao huu ulimshuhudia mmiliki wa duka hilo ambaye kwa ‘ubize’ wa tukio hilo hakuweza kuzungumzia tukio hilo kwani aliamua mara moja kuomba msaada kwa wananchi waliofurika katika eneo hilo walivunje boksi hilo pamoja na vioo hivyo kwa lengo la kumchomoa majerehi huyo.

Wananchi walimtoa kijana huyo akiwa ameshapoteza fahamu kufuatia kukatwa na vioo na kukosa hewa kwa muda aliokuwa amefunikwa na vioo hivyo.

Mwandishi wetu alizungumza na rafiki wa Dede aitwaye Dago Awadh ambaye alisema: "Mimi na Dede tulikodiwa na Mhindi huyo kumshushia mzigo wake huu na kwamba wakati tukihangaika, lori moja lilipita jirani ya Fuso hili hivyo mtikiso wake ulisababisha boksi hili kuyumba na Dede alipojaribu kujiokoa alitumbukia ndani na kujeruhiwa kama ulivyoona, " alisema Awadh.

Baada ya Dede kuchomolewa kwenye boksi hilo alikimbizwa hospitali na teksi iliyokodiwa na mwenye mali ambaye naye aliwasha gari lake na kueleka hospitalini.



0 comments: