




SHINDANO la kumsaka Kimwana Manywele Twanga Pepeta 2011, linazidi kutikisa jiji kufuatia washiriki wengi kujitokeza kuchukua fomu za kushiriki kwenye kinyang'anyilo hicho.
Baadhi ya washiriki wa shindano hilo walikutana na Waratibu wa shindano hilo jana ndani ya Ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam, na kupata kuzungumza macheche kuhusiana na utaratibu utakao tumika kwenye mazoezi yao.
Akizungumza na Mateja20, mratibu wa shindano hilo, Maimartha Jesse alisema kumba, tangu aanze kupokea fomu znazorudishwa na washiriki wa shindano hilo hadi sasa anazaidi ya fomu 50, na warembo ambao walijitokeza jana kwenye mazoezi ni zaidi ya ishirini.
Maimartha alisema, kufuatia wingi wa washiriki hao, watalazimika kuwa na mazoezi ya kila siku ili wapate kuwachuja kwa makini watakao ingia kwenye fainali ya kwanza inayotalajiwa kufanyika mei 6 mwaka huu, katika ukumbi wa Sun Cirro Club Ubungo jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment