
Huku shamrashamra za mkesha wa Sikukuu ya Pasaka leo zikiendelea, mtumishi wa Mungu mwenye ‘taito’ ya uchungaji katika kanisa moja la kiroho lililopo Kimara, Dar es Salaam (jina tunalo), aliyetajwa kwa jina moja la Glaba, anadaiwa kumpachika ‘kibendi’ msaidizi wa kazi za ndani ‘hausigeli’.
Tukio hilo la aibu kwa kanisa lilijiri hivi karibuni maeneo hayo ambapo mara baada ya kutenda dhambi ya kumpachika kibendi hausigeli aliyetajwa kwa jina la Rehema Yohane mwenye umri wa miaka 18, mchungaji huyo alitoroka na anasakwa kwa udi na uvumba jijini Dar ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Akilisimulia mkasa mzima ulivyomkuta akiwa nyumbani kwa muumini mmoja baada ya kutimuliwa na mwajiri wake kutokana na kupata ujauzito huo, Rehema alieleza kwamba, tangu alipotua Dar akitokea Dodoma mwanzoni mwa mwaka jana hajawahi kukutana kimwili na mwanaume mwingine zaidi ya mchungaji huyo.
Huku Rehema akiangua kilio kwa uchungu alisema: ”Cha kushangaza baada ya kitumbo kuchomoza, watu wamekuwa wakinifuata na kunipa pole wakiniambia mimba yangu haina mwenyewe kwa kuwa pasta huyo amekuwa na kasumba ya kuwarubuni mabinti kuwa atawaoa lakini akishapata ‘tunda’ huwapotezea.
“Pasta Glaba aliniambia yuko tayari kuishi na mimi lakini nasikia amemdanganya muumini mwingine kuwa anataka kumuoa wakati mimi nina ujauzito wake.
“Baada ya kuona msala unakua, nasikia jamaa ameuza kila kitu na kutokomea kusikojulikana, nilipomwendea hewani kumuuliza mbona amenikimbia, alinijibu ‘mbofumbofu’.
“Sasa mimba ina miezi mitano, nimeona niweke mambo hadharani ili pasta asiendelee kuwarubuni wanawake kwa kutumia dini.
Hata hivyo, Risasi Jumamosi lilifanya mahojiano na baadhi ya waumini wa kanisa hilo.
Mmoja wa waumini hao ambaye hakutaka jina lake lichorwe mateja20 alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli huyu mchungaji amekuwa akilaumiwa mara kwa mara kuwatundika vitumbo wanawake na kuingia mitini.
“Tena nasikia malalamiko kuwa wakati mwingine anafanya ngono ndani ya hekalu la Mungu (kanisa) akidai anawafanyia maombi ya ‘delivari’.
Muumini mwingine anayemfahamu Glaba kinagaubaga alidakia: “Siyo hapa tu, hata alipokuwa Morogoro aliwazalisha sana na hata jina analotumia si la ukweli, jina lake ni mchungaji Eliah.”
Juhudi za Risasi Jumamosi kumpata mchungaji huyo ziligonga mwamba kufuatia ‘laini’ zake tatu za simu kutokuwa hewani.
Kumekuwa na wimbi la watumishi wa Mungu kukumbwa na skendo chafu huku wakitumia jina la Mungu, hii ni ishara ya siku za mwisho.
0 comments:
Post a Comment