Social Icons

Tuesday, March 1, 2011

TEMBO ANAPOAMUA KUPAMBANA NA GARI!

Tembo aitwaye Amarula akianza mpambano dhidi ya gari hilo.
KATIKA tukio la kushangaza mpiga picha aliyekuwa amejificha pembeni, alichukua picha za dume la tembo ambalo lilipindua gari moja dogo "miguu juu" kama vile mwanasesere katika Mbuga za Wanyama za Pilansberg huko Afrika Kusini.

"Mpambano" huo kati ya tembo na gari hilo dogo ulianza wakati raia mmoja wa Ireland aitwaye John Somers, akiwa katika mapumziko ya kuadhimisha mwaka wa 66 tangu kuzaliwa kwake na wakati akipita katika bustani moja akiwa na rafiki yake, alipoamua kujaribu kumpita tembo mkubwa aliyekuwa mbele yake.

Hilo lilikuwa kosa baya, kwani tembo huyo aitwaye Amarula, mwanzoni alijipangusa kwenye gari hilo akifikiria ni tembo mwenzake mwanamke.

Lakini, muda mfupi baadaye mnyama huyo mkubwa akacharuka na kulipindua gari hilo ambapo watu waliokuwa ndani yake walijawa na hofu kubwa wasijue la kufanya.

Watu hao wawili waliokuwa ndani ya gari hilo, waliponea tundu la sindano ambapo walipata michubuko kadhaa kutokana na kitendo hicho.

Picha za tukio hilo zilipigwa na Riaan van Wyk, ambaye alikuwa akishuhudia tukio hilo kutoka mahali salama!




Mpambano huo ukiendelea raundi ya pili.

Gari likiwa limepinduliwa “miguu” juu.

0 comments: