Social Icons

Tuesday, March 1, 2011

KILI MARATHON YAFANA MOSHI

Emmanuel Nchimbi, akiwavisha medali washindi wa mbio hizo. Nyuma yake ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Tamasha la Kili Marathon ambalo huandaliwa kila mwaka na Kampuni ya Bia nchini ya (TBL), jana lilifana vilivyo katika viwanja vya Ushirika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Akiongea katika tamasha hilo, mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, alisema alifarijika kuona watu wengi waliojitokeza kujumuika katika tamasha hilo.

Nchimbi alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wote wa mchezo huo nchini na nchi za jirani waendelee kujitokeza kila mwaka ili waweze kukuza mchezo huo na kuufanya kuwa wa kimataifa zaidi.



Baadhi ya viongozi waliohudhuria tamasha hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi.

Waziri Nchimbi akiongea katika tamasha hilo.

Aliyekuwa mshiriki wa shindano la Bongo Star Search Joseph Pane, akitumbuiza kwenye tamasha hilo.

Kundi la TMK Wanaume Family likitoa burudani uwanjani.

Kiongozi wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Luiza Mbutu akiongea na mashabiki wa bendi hiyo.

Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakionyesha uwezo wao jukwaani.

Rapa wa Twanga Pepeta, Msafiri Saidi Sayai ‘Msafiri Diouf’ akionyesha makeke yake.

Mnenguaji wa Twanga Pepeta, Asha Sharapova, akiongoza safu ya wanenguaji.

Waimbaji wa Bendi hiyo, Charles Gabriel “Chalz Baba’ (kushoto), akiwajibika stejini na Dogo Rama (katikati), na mwishoni kulia ni Said Side.

Mpiga tumba wa bendi hiyo anayejulikana kama “MCD”, akiwa amemkumbatia mmoja wa wanenguaji wa bendi hiyo, Baby Face.

Baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo wakiwa wameuchapa usingizi kwenye basi walilokuwa wakisafiri nalo kuelekea Moshi katika tamasha hilo.

Mmoja wa waimbaji wa bendi hiyo, Dogo Rama, akiwa amejipaka sabuni usoni tayari kwa kujiweka sawa.

Baadhi ya wapiga vyombo wa bendi hiyo wakishuka katika basi muda mfupi baada ya kuwasili Moshi.

0 comments: