Social Icons

Sunday, March 20, 2011

KONDOO ALIYEANDIKWA KIARABU AKUTWA MSIKITINI MORO

Ustadh Hamisi Rajabu Dibagula ‘Mandela’ (mwenye shati jeupe na barghashia) akiwasomea watu alama alizokuwa nazo kondoo huyo.
Na Dunstan Shekidele,Moro
KONDOO aliye hai hivi majuzi amekutwa katika msikiti wa kijiji cha Msingizi, Wilaya ya Gairo, Mkoani Morogoro, akiwa ameandikwa maneno ya lugha ya Kiarabu.

Mbali na maandishi hayo upande mmoja wa mnyama huyo, upande wa pili ulikuwa na alama ya nyota ya pembe tano na maandishi yaliyosomeka ‘Lillah’ ambayo wataalam wa lugha hiyo walisema yanamaanisha “Mwenye kumilikiwa na Mwenyezi Mungu”.

Hivi sasa kuna juhudi za kumtembeza kondoo huyo katika misikiti mbalimbali mkoani Morogoro na hatimaye jiji la Dar es Salaam ili watu wamwone.

Juzi kondoo huyo alipelekwa msikiti wa 'Mungu Mmoja Dini Moja' wa Kiwanja cha Ndege, na jana alikuwa msikiti wa Luqman eneola Kihonda kwa Chambo ambapo leo alipelekwa msikiti wa Kichangani.

Msafara wa kumtembeza kondoo huyo uko chini ya kundi la Ustadh Hamisi Rajabu Dibagula 'Mandela'.

Alipotakiwa kuelezea namna alivyopatikana kondoo huyo, Ustadh Dibagula alisema mnyama huyo alizaliwa Novemba 17, mwaka jana katika kijiji cha Msingizi, Gairo, kwenye zizi la muumini wa dini ya Kikristo aliyejulikana kama Mzee Mdumbu na kwamba baada ya kuzaliwa alitoroka kwenye zizi hilo lililokuwa na kondoo na mbuzi.

Dibagula aliendelea kusema kwamba baada ya kutafutwa kwa muda kondoo huyo alipatikana katika msikiti huo na yeye (Dibagula) akaombwa na mashehe wa Gairo kumchukua baada ya Mzee Mdumbu kukataa kumpokea akihisi ni jini

"Mzee Mdumbu alihisi kondoo huyu ni jini baada ya kuona ana alama hizi,” alisema Dibagula.

Jana watu wengi walijazana katika msikiti huo wa Luqman kumshuhudia kondoo huyo, hivyo kusababisha vurumai kubwa na watu kupoteza vitu vyao.


Pia katika hafla hiyo, mtoto Adul Rashid (10) kutoka jijini Dar es Salaam alinogesha tukio hilo kwa “kumtambulisha” kondoo huyo kwa Waislamu na wasio Waislamu.

Zifuatazo ni picha zaidi za tukio hilo:

0 comments: