Social Icons

Sunday, March 20, 2011

ADONDOKA NA KUFA DAR

Polisi akimwangalia kwa makini marehemu.

MTU mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, amedondoka ghafla na kupoteza maisha papo hapo majira ya saa nne asubuhi ya leo maeneo ya Sinza A jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa shuhuda ambaye hakutaka jina lake litajwe, marehemu alianguka ghafla na alipomfuata na kumuuliza kilichomsibu hakuweza kuongea kwani meno yake yalikuwa yameumana na alikuwa akitetemeka.

“Nilikuwa pale nimesimama nikamuona huyu jamaa akianguka, nilipomfuata kujua kilichomsibu nikamkuta amekakamaa huku akiyabana meno yake. Nikapiga simu kuita polisi,” alisema shuhuda huyo.


Mwili wa mtu huyo ukibebwa kuingizwa katika gari la polisi.


Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.


Marehemu akiwa amefunikwa nguo.

0 comments: