Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Muganyizi Muta, akiwaonyesha waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam, baadhi ya makombe yatakayogombewa.
BENDI ya Msondo Music, Jumamosi hii inatarajiwa kutoa burudani katika bonanza la wanahabari lililoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel litakalofanyika viwanja vya Posta, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam. Katika bonanza hilo wanahabari watachuana katika michezo mbalimbali kama vile soka, kuvuta kamba na mingineyo ambapo zawadi mbalimbali yakiwemo makombe zitatolewa.
Mwanamuziki wa Msondo Music Band, Roman Mng’ande ‘Romario,’ akionesha baadhi ya manjonjo yake atakayoonyesha jukwaani.
0 comments:
Post a Comment