Kevin na Kate Rattray wakifurahia ‘mifugo’ yao nyumbani.
WANANDOA wawili wapenda wanyama huko Leeds, Uingereza, Kate na Kevin Rattray, wametenga chumba katika nyumba yao kwa ajili ya kufugia panya.
Watu hao wamedai wanapata furaha kubwa kuwaona panya hao wakipita huku na kule katika nyumba yao.
Jumla ya panya wote ni 28.Kwa watu wengine, kitendo cha panya kujaa nyumbani kingetosha kabisa kuita watu wanaojishughulisha na uuaji wa wanyama wadogo na wadudu katika majumba yao, lakini kwa wawili hao haikuwa hivyo.
“Wanatufurahisha kuwaona,” alisema Bi Rattray (31) alipoulizwa kuhusu hali hiyo ambapo aliongeza: “Ni wanyama wenye akili ambao hujitokeza kutupokea kwenye baa ya ndani ya nyumba yetu tunaporudi kazini.
Hatuoni shida kuwa nao. Wana tabia nzuri na inafurahisha kuishi nao.”
Kate alianza kuwapenda panya akiwa chuo kikuu ambapo alikuwa nao wawili, jambo ambalo mumewe hakulipenda.
Hata hivyo, mwaka 2006, baada ya Kevin kubadili mawazo, alianza kufuga panya.Hata wageni wao ambao walikuwa hawawapendi panya hao, walianza kuwazoea na kucheza nao.
Rattray, ambaye ni msimamizi wa maabara moja, na mkewe, wote ni wanachama wa klabu ya panya ijulikanayo kama Yorkshire Rat Club.
Watu hao wanaoishi Leeds, watatokea katika filamu ya kituo cha Channel 4 iitwayo – First Cut: Head Over Heels In Rats itakayoonyeshwa Ijumaa ya Januari 28 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment