Social Icons

Monday, January 17, 2011

YANGA ,ATLETICO KUKIPIGA KESHO

Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd , Rahma Al Kharmous, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Yanga ya jijini na Atletico Paranaense ya nchini Brazil, unaotarajia kuchezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Katikati ni Rais wa Klabu ya African Lyon, Nabil Salum, wenyeji wa ujio wa timu hiyo, na Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Kostadic Papic na kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri
Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd , Rahma Al Kharmous (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na makocha wa Klabu za Yanga, Simba na Atletico, baada ya mkutano huo leo.
Kutoka (kulia) ni Mratibu wa Masuaka ya Kimataifa wa Klabu ya Atletico Paranaense,Frank Romanoski, Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd, Rahma Al Kharmous, Rais wa Klabu ya African Lyon, Nabil Salum, kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Kostadic Papic na Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Patrick Phiri, wakifurahia Skafu ya Klabu ya Atketico, baada ya kukabidhiwa na viongozi wa klabu hiyo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam leo

0 comments: