Rais wa Shimbata, Monday Likwepa, akimkabidhi fulana yenye nembo ya shirikisho hilo, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Mwanaidi Shemweta. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Dk. Anna Senkoro. NIC ni mmoja wa wadhamini wa shirikisho hilo.
SHIRIKISHO la mchezo wa bao Tanzania (Shimbata) leo limetangaza kuundwa na kusajiliwa rasmi kwa vyombo vya habari kwenye mkutano wake na wanahabari uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari ‘MAELEZO’ jijini Dar es Salaam. Hivi karibuni shirikisho hilo linatarajia kumkabidhi bao mlezi wake mpya mama, Salma Kikwete.
0 comments:
Post a Comment