Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Anne Makinda (wa pili kulia) akiwa pamoja na Maspika wenzake kutoka katika mabunge ya nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Madola ambao wanaunda Kamati Tendaji. Maspika hawa wanakutana katika kisiwa cha Isle of Man kilichoko chini ya utawala wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kuandaa mkutano wa wanachama wote utakaojadili mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupanda kwa bei za vyakula ulimwenguni. Kikao hicho kilichoanza tarehe 12 kitakamilika tarehe 15 Januari 2011. Spika Makinda atarejea nyumbani tarehe 16 Jan. 2011. Hapa maspika wako kwenye tafrija iliyoandaliwa kwa heshima yao.
Maspika wakitembelea maeneo mbalimbali ya kihisoria katika Kisiwa cha Isle of Man.
Spika Makinda akiwa na Spika wa India Mhe. Meira Kumar (kati) katika mkutano huo.
Picha zote na Prosper Minja wa Bunge
0 comments:
Post a Comment