Hi Global Publisher Team!
First of all I would like to take this oppurtunity to congratulate you all for the good work that you do.
Mimi ni mtanzania mwenye kuipenda nchi yangu. Nyinyi kama waandishi wa habari, nimeona nikuandikieni jambo ambalo linanikera kweli kweli, tena linanikereketa vibaya vibaya na kufanya nione aibu. Ni kuhusu film zetu za kibongo ambazo zinaonyeshwa na DSTV kwenye Channel 115 Africa Magic Plus. Hizi film hufanyiwa translation kwa kuwekwa sub-titles za English, kwa vile film zenyewe huwa ni za Kiswahili ili watu kutoka nchi nyengine waweze kuelewa kinachoendelea kwenye hizo film.
Kilichonifanya haswa kukuandikieni hii email ni kuwa nyingi ya hizi film translation yake inakuwa sio sahihi, kwanza kabisa kingereza kibovu, wrong spelling. Kwa mfano kama jana tarehe 12 January 2011 niliangalia film inaitwa Chozi la Yatima - aibuuuuuu ndugu zangu manake hicho kingereza ovyoooo na spelling ni hivyo hivyo. Mfano jamaa anasema kuwa anaenda kukata ticket ya kusafiria airport basi translation imeandikwa "I am go to cut ticket at the airport"
My goodness! My English is not the best in the country but its a pity that this channel is watched by people all over Africa and may be beyond and its an embarrasement to all of us.
Nnahakika kuwa mnaweza kulizungumzia hili suala ili wahusika wasikie na watafute watu ambao watafanya kazi kwa ufasaha sio akina sie tuliosomea kingereza vichochoroni na kujiona kuwa tunakijua sana hadi kutaka kufanya translation kazi kubwa kama hizo ambazo zinafika mbali.
I hope that I have been heard by your team and I am hereby hoping that you will do the necessary so as to potray good work that comes from Tanzania that is being presented well inside and outside Tanzania. Yes we Can !
Remain Blessed
0 comments:
Post a Comment