Asalaam alaykhum,
WAPENZI WA BLOG YA CHAKULA BORA NA SALAMA NAFURAHA KUWAPATIA TAARIFA HIZI RASMI TOKA BLOG HII TOKA ILIPOANZA MWAKA JANA MWEZI WA KWANZA MPAKA LEO TUMETOKA WAPI NA TUNAKWENDA WAPI NA NINI MALENGO KWA MWAKA MPYA.
(KWANZA KABISA NAWASHUKURU SANA RAFIKI WOTE NILIOWEZA KUONANA NA WENGINE KUONGEA NAO KATIKA SIMU KIPINDI NIKIWA DAR ES SALAM WAKATI WA MWAKA MPYA TULIWEZA BADILISHANA MAWAZO NA NIKASIKILIZA MICHANGO YENU YOTE NITAYAFANYIA KAZI.
NILITOA SWALI KABLA YA MWAKA MPYA ILI MSHINDI AWEZE JIPATIA ZAWADI INGAWA SIKUTAJA NI ZAWADI GANI. MSHINDI HAKUWEZA KUPATIKANA KWAKUA SIKUWEZA PATA JIBU SAHIHI WENGI WENU MLIKARIBIA JIBU.
JIBU SAHIHI ILIKUA NI .... TAR 1/1/2010 NDIO BLOG YETU ILIANZA RASMI KWAHIYO TAR 1/1/2011 BLOG INAFIKISHA MWAKA MPYA NA ILITAMBULISHWA RASMI KATIKA MICHUZI BLOG.
SINA BUDI KUWASHUKURU SANA BLOG WANACHAMA WALIOSAIDIA SANA KUWAFAHAMISHA WASOMAJI UWEPO WA BLOG HII IHUSUYO MAPISHI NA WASOMAJI KUIPOKEA KWA MIKONO MIWILI. SIKU IMEFUNGULIWA ILIPATA WASOMAJI 600 NA BAADA YA SIKU 3 ILIKUA INAWASOMAJI 6000. KWA KIPINDI CHA MWAKA MZIMA BLOG IMEWEZA PATA WASOMAJI 140.000 TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA NA WAFUASI HALISI ZAIDI YA 90.
NAWASHUKURU SANA WASOMAJI WOOTE KWA KUNIPA MOYO NA KUSHUKURU KWA KUFAIDIKA NA MAFUNZO PIA KUNIPA MAWAZO NA MENGI NAYAFANYIA KAZI INGAWA MENGINE YANAKUA NJE YA UWEZO WANGU.
SHUKURANI ZA DHATI ZIWAENDEE MICHUZI BLOG, DJ CHOKA, 8020FASHION, JIACHIE BLOG NA GLOBAL PUBLISHERS KWA MSAADA NA MCHANGO WAO MKUBWA.
MIPANGO YA MWAKA HUU NA KUENDELEA
NAJITAHIDI NIWEZE TENGENEZA VIDEO FUPI ZA MAFUNZO YA MAPISHI ILI ISAIDIE KUELIMISHA ZAIDI KWA MIFANO. PIA NIMEANZA KUANDAA KITABU CHANGU CHA MAPISHI NI KAZI NGUMU NA KITACHUKUA MUDA LAKINI NAIMANI KITAKAPO KAMILIKA MTAFURAHIA SANA LENGO KIWE KATIKA LUGHA YA KISWAHILI NA LUGHA YA KIINGEREZA KUZINGATIA ZAIDI USHAURI WA KIAFYA KWA CHAKULA BORA.
MAFUNZO YANAENDELEA NAHITAJI SANA MASWALI NA MICHANGO YA MAWAZO TOKA KWENU ILI KILA MMOJA WETU AFAIDIKE NA TAALUMA HII.
NAWATAKIA KAZI NA SIKU NJEMA
CHEF ISSA
Tuesday, January 18, 2011
TAARIFA RASMI YA MWAKA MZIMA
Labels:
www.mateja20.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment