Zungu akiongea na wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Azzan Zungu, leo amekabidhi madawati kwa Shule ya Chekechea ya Mwangaza iliyopo Kigogo Sambusa, Kata ya Mchikichini, jijini Dar es Salaam.
Makabidhiano hayo yalifanyika leo majira ya saa nne na nusu asubuhi ambapo mbunge huyo aliwataka wazazi kuichangia shule hiyo badala ya kutegemea michango kutoka kwa wafadhili.
Zungu (kulia) akipeana mikono na Diwani wa Kata ya Mchikichini, Riyami Gharib Abdallah, mara baada ya kukabidhi madawati hayo.
…Akiwa amekaa katika moja ya madawati hayo na baadhi ya wanafunzi pamoja na mwalimu wa shule hiyo (Kulia)
Baadhi ya wazazi na wanafunzi hao wakimsikiliza Zungu.
Wanafunzi wakisubiri ujio wa Zungu shuleni kwao.
0 comments:
Post a Comment