Social Icons

Thursday, January 6, 2011

CHADEMA POLISI ARUSHA KWAWAKA MOTO

JIJI la Arusha hali si shwari baada ya askari wa kutuliza ghasia kufyatua risasi za moto na kutupa mabomu ya machozi katika maeneo ya Kata ya Kati mjini na kusababisha wakazi wa mitaa na maeneo ya stand kutokwa na machozi hovyo na wengine kufunga maduka huku vilio vya watoto wadogo vikitawala.
Mabomu hayo yaliendelea kulipuliwa katika maeoe kadhaa kuanzia saa 6 mchana hadi saa 11 jioni, hatua ambayo ilisababisha shughuli zote za maendeleo, wasafiri, watoto waliokuwa wanakwenda shule kusitisha huduma zote.

Baadhi ya wanachama wa CHADEMA wakiwa na mabango yenye ujumbe wakati wa vurugu hizo.
Wakijiandaa kwa maandamano...
Baadhi ya wanachama wakipakiwa katika gari la Polisi baada ya kukamatwa kwenye vurugu hizo.

Chanzo sufianimafoto blog

0 comments: