Mtangazaji wa mchakato huo, Godwin Gondwe (kushoto), akimkaribisha kuongea na majaji mshiriki wa kinyang’anyiro hicho, Christ Bella Nzowa, (kushoto) ni mpigapicha wa kipindi hicho akiwajibika.
Kama kawaida ya kamera yetu usiku wa kuamkia leo ilizama ndani ya Ukumbi wa Water Front Posta jijini Dar es Salaam,ambapo ilibahatika kushuhudia maandalizi ya kipindi hicho na kupata baadhi ya matukio laivu ambayo yanatarajiwa kurushwa hewani Jumapili kupitia Kituo cha Runinga cha ITV.
Jaji mkuu wa kinyang’anyiro hicho, Lita Paulsen ‘Madam Lita’ (kushoto), akiwa kwenye pozi na jaji mwenzake, Salama Jabir (katikati), mwisho kulia ni Mtangazaji wa Shindano hilo, Godwin Gondwe ‘Double G’
Majaji wa mchakato huo wakichakachua kura tayari kwa kutoa matokeo kwa wanaoliaga shindano hilo.
Baadhi ya wapiga picha wakiwajibika.
Washiriki wote kumi wakiwa kwenye pozi la pamoja tayari kwa kutajwa majina ya watakaoaga kwenye mchuano huo.
Bella Kombo akiangalia runinga kwa machungu muda mfupi baada ya majina ya ‘waliochapa lapa’ kutajwa.
Mariam Mohamed akiangua kilio baada ya washiriki wenzake kutupwa nje ya kinyang’anyiro hicho.
Joseph Pain naye akisikilizia kwa machungu majina ya walioaga shindano hilo.
0 comments:
Post a Comment