Rehema Fabian (kushoto), akishusha mizigo kwenye gari lake tayari kwa kutoa msaada. Kulia ni mlinzi wa kituo hicho akibeba baadhi ya mizigo iliyotolewa.
Mshiriki wa kinyang’anyiro cha Miss Kiswahili 2008/09, Rehema Fabian, mapema leo amemwaga misaada yenye thamani ya shilingi laki tatu (300,000/=) katika kituo cha kulelea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
Miss Kiswahili akimbebesha moja ya mizigo hiyo mtoto wa kituo hicho.
Rehema akigawa Pipi kwa watoto hao.
Rehema akimuandalia Pipi mmoja wa watoto wa kituoni hapo.
Rehema akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima.
Katibu Mtendaji wa kituo hicho, Hassan Hamis (kushoto), akiagana na mrembo huyo baada ya kumaliza kutoa misaada hiyo
0 comments:
Post a Comment