Mhamasishaji, Mjasiriamali na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akiongea na wasomi wa Chuo Kiuu Dar es salaam -Mlimani.
Mjasiriamali anaye fahamika zaidi kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa watu kwa lengo la kujikomboa na umasikini, Bw Eric James Shigongo, mapema leo ameongea na wasomi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara na kuteka hisia zao baada ya kutoa mafundisho ya jinsi ya kujikomboa na umasikini.
Katika hotuba yake, Shigongo ambaye hivi sasa ametoa DVD ya ujasiriamali iitwayo Street University, aliwaambia wanachuo hao kwamba maisha ya siku hizi si ya kutegemea ajira peke yake, badala yake wajenge kanuni za kujitegemea kama wajasiriamali kwa lengo la kujenga nchi ya wajasiriamali wengi.
“Lazima tujenge mawazo ya kujitegemea badala ya kusubiri serikali itufanyie kila kitu, sasa mko chuoni naomba mkayafanyie kazi kwa vitendo yale mnayojifunza hapa chuoni,” alisema Shigongo na kuongeza;
“Mafanikio yanawezekana kwa kila mmoja endapo tu ata amua, hakuna mtu aliyezaliwa kuwa masikini wala tajiri, bali vyote hivi tumevikuta diniani na tunavipata kutokana na jinsi tunavyofanya mambo maishani”
Pamoja na Bw. Shigongo, mota mada mwingine aliyekuewpo ni Bw. David Mgwasa kutoka kiwanda cha Tanzania Breweries Limited (TBL) ambaye aliwasisitizia wasomi hao kutokuwa na mawazo tegemezi hata mara baada ya kuhitimu masomo yao.
Bw. David Mgwasa kutoka TBL naye akitoa mada
Korosso Undule, Mwenyekiti wa wanafunzi - Kitivo cha Biashara akiongea kwenye mkutano huo
Bw. Geofrey Tangamana, Mshauri wa Mambo ya Fedha Kitivo cha Biashara, akitoa mada
...waalikwa wakishangilia mada ya Bw. Shigongo
Bw. Shigongo akihamasisha waalikwa
...vijana wa chuo wakibadilishana mawazo na Shigongo nje ya ukumbi mara baada ya mkutano
baadhi ya wasomi Kitivo cha Biashara wakiwa katika picha ya pamoja na Shigongo.
0 comments:
Post a Comment