Social Icons

Monday, December 6, 2010

WALTER WA TBS1 APATA JIKO!!!


Walter akiwa katika pozi na mkewe Adelaida.

MFANYAKAZI wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), ambaye pia alikuwa Mfanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Walter Rumisha Maleko, juzi alifunga ndoa na Adelaida ambaye ni Mfanyakazi wa Benki ya Akiba. Harusi hiyo ya aina yake ilifungwa katika Kanisa la Azania Front, Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mamia ya watu na sherehe ilifanyika katika ukumbi wa Lion uliopo Sinza, Jijini Dar es Salaam.


Bibi Harusi Adelaida, akimlisha keki mumewe Walter, pembeni kushoto aliyesimama ni mama yake mzazi Walter.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Global waliohudhuria sherehe hiyo wakiwa katika pozi, kutoka kushoto ni: Rhobi, Bahati na Edna.


Mtaalam wa IT wa Global Publishers, Clarence Mulisa (kulia) akiwa na mfanyakazi mwenzake wa kitengo cha Graphic Designer, George Alphonce 'MC George' katika sherehe hiyo.


Mhariri Kiongozi wa Gazeti la Championi, linalochapishwa na Global, Saleh Ally, akiwa na wife wake Sarah katika harusi hiyo.


Mc wa sherehe hiyo, Godwin Gondwe 'Double G' akiwa mzigoni.


Ndafu aliyeandaliwa kwa sherehe hiyo akikatwa tayari kwa kitoweo.


Wafanyakazi wa Global Publishers, wakiongozwa na Clarence pamoja na Rhobi wakipeleka zawadi kwa maharusi.


Walter na Adelaida wakifungua muziki.


Wafanyakazi wa Global, Rhobi Chacha na Clarence wakitoa burudani.


Mc George akicheza muziki pamoja na maharusi.

0 comments: