KAMPUNI ya Feyak Co.Ltd ya jijini Dar es Salaam leo wameandaa maonyesho ya wanafunzi wa shule za chekechea, msingi na sekondari yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mlimani City. Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jane Tesha amesema kuwa wameamua kuandaa maonyesho hayo ili iwe rahisi kwa shule mbalimbali kufahamika zaidi katika suala zima la ufundishaji wao pamoja na ufanisi. PICHANI Mkurugenzi wa Feyak Company Limited, Jane Tesha akitoa maelekezo mafupi kwa Naibu Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Sarah Ndaba (mwenye Singlend ya kijani).
Muuzaji wa DVD za STREET UNIVERSITY akionesha bidhaa zake katika viwanja hivyo.
Mteja wa DVD ya STREET UNIVERSITY akiweka sahihi katika kitabu maalum baada ya kuinunua.
moja wa wanafunzi wa shule ya Chekechea ya Tusiime ya jijini Dr es Salaam akitoa maelekezo kwa mmoja wa watazamaji waliohudhuria maonyesho hayo.
0 comments:
Post a Comment