Social Icons

Monday, December 13, 2010

KILIMANJARO STARS WALIPO TINGA IKULU

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, wakimsubiri Rais. Jakaya Kikwete katika hafla ya kuwapongeza.


TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars leo imetinga Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hafla ya kupongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete kwa kufanikiwa kutwaa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Katika mechi ya fainali iliyochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Kili ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 kupitia mkwaju wa penalti iliyopigwa na Shadrack Nsajigwa baada ya beki wa Ivory Coast kuunawa mpira katika eneo la hatari.

Zifuatazo ni picha zinazoonesha mambo mbalimbali yaliyojiri katika huko ikulu.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga akiteta jambo na Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Jan Poulsen wakati wakimsubiri Rais Kikwete.

Rais Kikwete, Leodegar Tenga na baadhi ya wachezaji wa Kili Stars wakiliangalia Kombe la Chalenji ambalo timu hiyo imefanikiwa kulitwaa Jumapili iliyopita kwa kuinyuka Ivory Coast bao 1-0.

Nahodha wa Kili Stars, Shadrack Nsajigwa akimkabidhi kombe hilo Rais Kikwete.

Rais Kikwete akiwapongeza wachezaji hao.

Baadhi ya wachezaji wa Kili Stars na viongozi wa timu hiyo huku mbele yao kukiwa na Kombe la Chalenji leo mchana.

0 comments: