Baadhi ya wanamuziki wa zamani wakiwa nyumbani kwa marehemu Ongala leo mchana.
BAADHI ya wanamuziki wa zamani wa muziki wa dansi waliokusanyika nyumbani kwa marehemu Remmy Ongala wamesema kuwa watatunga wimbo wa kumuenzi mwanamuziki huyo aliyefariki usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda.

Waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu eneo la Sinza.

Wanamuziki wa zamani, Abdul Salvado ‘Fadha Kidevu’ (kushoto) akiwa na Hamza Kalala wakiongea na mwandishi wetu (hayupo pichani) jinsi walivyoupokea msiba huo kwa mshituko mkubwa.
0 comments:
Post a Comment