Kibaka mtuhumiwa akipata kichapo ‘kitakatifu’ kutoka kwa mwananchi.
JAMAA mmoja aliyedhaniwa kibaka hivi karibuni alinusulika kufa baada ya kupokea mkong'oto mkali toka kwa wanachi wenye hasira wa eneo la Mbande njia panda ya kuelekea Wilaya ya Mpwapwa na barabara kuu ya kwenda Dodoma baada ya kumkamata akijaribu kumchomolea fedha mfanyabiashara wa mahindi.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo waliueleza Mtandao huu kwamba kibaka huyo alijalibu kumchomilea pochi mfanyabiaashara mmoja wa mahindi aliyekuwa akila Chipsi katika eneo hilo.
Kibaka mtuhumiwa akiendelea kupata kichapo.
"Kuna mfanyabiasha wa mahindi ambaye alisimama eneo hili kwa lengo la kupata riziki na kwamba kibaka huyo baada ya kumuona mfanyabiashra huyo ambaye mifuko yake ilikuwa imetuna kwa wingi wa pesa alisogea jirani naye na kuanza kujaribu kumchomoa pesa kiasi ambazo zinakadiriwa kuwa shilingi milioni moja na nusu.
“Jamaa alimstukia na kuanza kupiga kelele za mwizi ambapo watu wengi waliokuwepo eneo hili walimzingira kibaka huyo na kuanza kumpa mkong'oto mkali," alisema mmoja wa mashuhuda hao aliyegoma kutaja jina lakeKibaka mtuhumiwa akiwa hoi baada ya kupata kichapo.
Kibaka huyo alitumia janja ya njyni baada ya kuona kipigo kinazidi alijikausha na kujifanya amekufa na kwamba wanachi hao baada ya kuona hali hiyo mmoja mmoja walisepa wakihofia mkondo wa sheria wakidhani kibaka huyo ameshakufa.
Baada ya muda kibaka huyo alizinduka na kutimua mbio huku akivuja damu mwili mzima.
0 comments:
Post a Comment