Social Icons

Sunday, December 5, 2010

BIBI AKIKOMAA NA ICE CREAM

Katika pitapita zake, mpiga picha wetu alikutana na bibi Asha Salum (pichani, juu na chini) maeneo ya Mji Mpya mjini Morogoro akilamba 'ice cream' ambayo kwa kawaida hupendwa sana na watoto. Bi Asha alimwambia mpiga picha wetu kuwa alimua kulamba 'asikirimu' ili kupoza koo baada ya kusikia kiu kutokana na jua kali na mwendo mrefu. Bibi huyo alidai alikuwa ametoka mjini kutafuta dawa ya Malaria, lakini alishindwa kununua kutokana na kuwa ghali, aliahidi kurudi nyumbani na kutafuta dawa za mitishamba kutibu malaria yake ambayo imekuwa ikimsumbaua kwa muda wa wiki moja sasa.

0 comments: