Wafanyakazi wa Kampuni ya Majembe wakisikiliza jambo kwa makini.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) leo limeingia mkataba na Kampuni ya Majembe inayojihusisha na ukusanyaji madeni na kupiga mnada vitu mbalimbali kwa ajili ya kufanya kazi ya kusajili kumbi mbalimbali za starehe ambazo hazijasajiliwa.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Basata, Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego alisema kutokana na tamko lililotolewa na serikali la kusajili kumbi zote za starehe ili kutokomeza vitendo vya uhalifu, baraza hilo limeamua kufanya kazi pamoja na Kampuni ya Majembe ‘Vijana wa kazi’ kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja ambapo wataanza kazi mara moja.

Katibu Mtendaji Basata, Ghonche Materego akisaini mkataba kwa ajili ya kuukabidhi kwa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Majembe, Seth Motto akisaini mkataba kwa ajili ya kuukabidhi kwa Katibu Mtendaji wa Basata.
Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego (kulia) wakikabidhiana mkataba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Majembe, Seth Motto (kushoto).
0 comments:
Post a Comment