Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za mkononi ya Zain Tanzania, mapema leo imezindua jina jipya ambapo sasa itajulikana kwa kwa Jina la Airtel. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, majira ya saa nne asubuhi na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Sam Elangalloor alisema kuwa, wameamua kuzindua chapa yake ya kimataifa ili kuunganisha shughuli zake kwa wateja barani Afrika ambapo wateja wake wote wataweze kufaidi viwango sawa. Pichani: Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor (katikati), akiwa ameshikilia Logo mpya tayari kwa uzinduzi huo Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Miradi na Maendeleo Afrika, Steve Torode na mwisho ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Cheikh Sarr.
Wakurugenzi Airtel Tanzania wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Cheikh Sarr akifafanua jambo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor akielezea utaratibu mzima wa zoezi hilo.
eneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Mutta Mganyinzi wa (pili kushoto) akifuatilia mchakato huo na wandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Baadhi ya Wanahabari wa vyombo mbalimbali nchini wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.
Logo mpya ya Airtel
Zain Afrika yawa Airtel
• Airtel yazindua chapa yake ya kimataifa ili kuunganisha shughuli zake barani Afrika
• Wateja wote kufaidi viwango bora zaidi vya huduma, bunifu na nafuu kokote walipo, nyumbani, kazini na hata safarini.
Dar es salaam- Novemba 22, 2010: Bharti Airtel, moja kati ya kampuni tano kubwa za mawasiliano ya simu duniani, leo imetangaza kuzindua chapa yake mpya ya kibiashara barani Afrika, kwenye nchi 15 ikiwemo Tanzania,kutoka Zain ambayo ilinunuliwa mwezi wa Juni, 2010 na sasa kuwa Airtel.
Kuanzia sasa, Airtel ndilo litakuwa jina la utambulisho wa kampuni, Afrika na Asia, katika nchi 19 pamoja na bidhaa mbalimbali pia zitabadilishwa , lengo likiwa ni kuweza kuwafikia wateja wote kwa kutumia jina moja imara. Pia, huduma huduma za kampuni na bidha mpya na za kibunifu zitabadilishwa ili kushabihiana na chapa ya kibiashara ya Airtel. Huduma ya kutuma na kupokea fedha ya “ZAP” kuanzia sasa itaitwa ‘Airtel Money’.
Manoj Kohli, Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Pamoja wa Bharti Airtel Afrika nzima, amesema: "Airtel inafikisha kwa pamoja shughuli zote zetu chini ya utambulisho mmoja, wa chapa imara na ya kipekee. Tunaweza kuwafikia zaidi wateja wetu zaidi kwa kuendesha kwa utambilisho wa chapa ya aina moja barani Afrika ili kukidhi ahadi yetu ya kutoza viwango na gharama nafuu zaidi vya mawasiliano ikiwa ni pamoja na huduma zenye ubunifu wa hali ya juu kwa wateja wet utendaji kama lengo ni moja katika Afrika; kutimiza ndoto yetu ya kutoa gharama nafuu na huduma za simu kwa ubunifu kwa ajili ya wote.
"Wateja wetu watakuwa na huduma nzuri kama walivyozoe kutoka kwetu na kufurahia kiwango vya juu zaidi vya huduma, vyenye uhakika, bunifu na nafuu zaidi ama wakiwa katika makazi yao, kazini ama safarini. Pia Aitel inalenga kuleta maendeleo zaidi katika sekta ya mawasiliano kwenye nchi zote tunazoendesha bishara ya mawasiliano kwa kupanua zaidi wigo wa mtandao wetu kuelekea katika maeneo ya vijijini na pia kupitia mpango wetu wa kusaidia sekta ya elimu”.
Kwa mujibu wa ripoti ya Deloitte, kwa kuratibiwa na Muungano wa Sekta ya Mawasiliano ya Simu (GSMA), ni asilimia 40 tu ya waafika wote ndie wenye uwezo wa kimiliki simu za mkononi, na kwa ongezeko wa asilimia 10 tu kwa kila mwaka, linaweza kuchangia kuinua pato la ndani la taifa kwa asilimia 1.2 katika nchi zinazoendelea.
Mahitaji yameonyesha kuongezeka kwa kiwango cha wastani wa asilimia 25 kwa mwaka, na wachambuzi wanabashiri ya kwamba barani Afrika, hususani kusini mwa jangwa la Sahara, hadi kufikia mwaka 2013, kutakuwa na ongezeko la watumiaji wa simu za mkononi hadi kufikia asilimia 65, wengi wao wakitoea maeneo ya vijijini.
Sam Elangalloor, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania amesema: "Tunadhamiria kuongeza idadi ya wateja wetu kwa asilimia 150 barani Afrika ifikapo mwaka 2012 na kuweza kufikia wateja milioni 100 katika bara zima. Ukuaji huo utachochea uchumi na kujenga maelfu ya ajira za moja kwa moja; ajira kupitia wadau wa mauzo na usambazaji na hata kuweza kuunganisha jamii”.
"Siyo tu kwamba tutachangia katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania, bali pia tutasaidia watanzania kutimiza malengo yao mbalimbali kupitia mawasiliano ya simu za mkononi ambayo ni bunifu, mahususi, yenye kupatikana kwa uhakika na yaliyo nafuu”.
Kwa muda wa miezi mine iliyopita, Airtel tayari imefanya mabadiliko makubwa katika viwango vya mawasiliano kwenye soko la nchi 11 kati ya 16 barani Afrika, kwa lengo la kuwanufaisha wateja. Pia imeingia makubaliano na kammpuni tatu kubwa ulimwenguni katika huduma za miundombinu ya mawasiliano – Errickson, Huawei na Nokia Seamens – ili kusambaza na kuweza kufikisha huduma zake katika anga za mbali zaidi, hususani maeneo ya vijijini ambayo kwa sasa yanakabiliwa na changamoto na uhaba wa mawasiliano ya simu. Naye Sheikh arr, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, amesema: " ni matarajio yetu kuwa simu za mkononi zitakuwa daraja muhimu la kuunganisha jamii na teknolojia ili kubadilisha maisha ya watu katika bara la Afrika kwa ajili ya ubora, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuunganisha watu na ulimwengu, wengine ikiwa ni mara ya kwanza kabisa – na kuwapa wengine fursa zaidi katika elimu, afya na huduma za kibenki popote walipo.
Upatikanaji wa mawasiliano ya simu kutawapa watu uhuru wa kufikia malengo yao katika maisha, kubadilisha jinsi watu wanavyowasiliana na jinsi jamii inavyotenda kazi yake .Kukamilisha ahadi ya kuwezesha mawasiliano simu zitapatikana kwa gharama nafuu na kwa kila mtu”.
Simu za mkononi za bure kwa ajili ya wote
Ikiwa ni kutimiza ahadi ya kuleta unafuu katika mawasiliano ya simu za mkononi kwa kila mtu, Airtel pia imetangaza kuanza kuuzwa kwa simu za viwango nafuu kabisa ambapo mnunuaji analipia gharama za mawasiliano pekee huku simu ikiwa ni ya bure.
Katika mpango huu uliozinduliwa, ambao ni kwa kushirikiana na Nokia, kwa kiasi cha Shilingi 39,000, mteja wa Airtel anapata simu ya Nokia 1280, laini ya SIM pamoja na muda wa maongezi pamoja na SMS gharama hizo hizo.
Sam Elangalloor, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, alisema: "Tunasukumwa zaidi na dira yetu ya kufanya mawasiliano ya simu kuwa nafuu na kupatikana kwa wote. Urahisi katika kupata mawasiliano ya simu kutawapa watu uhuru zaidi wa kufikia malengo yao katika maisha, kubadilisha jinsi watu wanavyowasiliana na hata kurahisisha mawasiliano baina ya wanajamii.
"Tunaamini kuwa kwa sisi kuleta fursa hii katika sekta ya mawasiliano, ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa kila mtanzania anawezeshwa kuwasiliana ka njia ya simu, hata Yule aliye na hali ya chini kabisa na walio maeneo ya ndani zaidi ya nchi”.
Ubunifu waleta mabadiliko
Ni dhamira thabiti ya Airtel katika kutoa suluhisho mahsusi na lenye ubunifu wa hali ya juu katika sekta ya mawasiliano nchini , ili kuweza kuongeza ufanisi katika maendeleo ya jamii na uchumi kwa watanzania.
One Network, muundo wa mawasiliano bila kikomo ambao unaongoza duniani, utaendelea kuwa nguzo muhimu na imara kutoka Airtel, kama ambavyo umetambulika ulimwenguni kote kama mfano wa kipekee wa maendeleo ya teknolojia katika sekta ya mawasiliano, kwa mujibu wa Vivienne Redding, kiongozi wa zamani wa Kamisheni ya Ulaya.
Ikiwa inapatikana katika nchi 26 barani Afrika na Mashariki ya Kati, Airtel One Network inawawezesha wateja wa malipo ya kabla na ya baada, kuweza kuvinjari katika nchi zote zilizounganishwa kwa pamoja, wakiwa huru na bila ya kuhitaji kulipia simu zinazoingia.
Wateja pia hupata huduma nyingine kama wanavyokuwa nchini kwao kama voicemail na huduma kwa wateja katika lugha zao nchini kwao, na mawasiliano ya kuhamisha mikopo kwa ajili ya wateja wa kulipia kabla.
Pia, wateja wa Airtel, wawapo nchi nyingine kwa kupitia One Network, wataendelea kupata na kufurahia huduma sawasawa na zile walizokuwa wakizipata kupitia nchi walizotokea. Hii ni pamoja na Ujumbe wa Sauti, huduma kwa wateja kwa lugha ya nchi aliyotokea, kutuma na kupokea salio kwa wateja wa malipo ya kabla.
"kihistoria kanda iliyozoea uhuru wa kuvuka mipaka, huduma hii inafaa mahitaji ya wateja wetu kikamilifu, kuvunja vizuizi na kufanya maisha bora kwa ajili ya biashara, familia na watu binafsi kutoka Atlantiki na Bahari ya Hindi," alisema Manoj Kohli .
Chapa Mpya
Chapa mpya ya kibiashara ya Airtel ni zaidi ya mabadiliko ya jina. Alama ya kibiashara inaingiakatika soko huku ikitimiza ahadi ya kukidhi mahitaji ya wateja, kuleta ubunifu, unafuu wa gharama na muhimu zaidi kuwapatia wateja uhuru kuchagua huduma na bidhaa za mawasiliano kulingana na mahitaji yao ya kila siku.
Rangi nyekundu, ambayo ndiyo rangi kuu ya chapa ya Airtel, inaashiria utulivu na msisimko wa bara la Afrika. Ni rangi yenye kuashiria uhai barani Afrika, mithiri ya jua linalochwea. Sifa hizi zote zinaitambulisha Airtel kama chapa imara, madhubuti na iliyo tayari kujitolea.
muundo na utambulisho wa chapa hii mpya umetengenezwa kwa ushirikiano na ubia wa makampuni ya WPP, kampuni kubwa duniani ya masoko. Brand Union wamehusika na kutengeneza utambulisho, Millward Brown ilifanya utafiti na kukusanya maoni ya wateja; Ogilvy maendeleo ya 360 shahada ya kampeni, na Hill & Knowlton iliyoongoza mawasiliano.
Mbunifu wa chapa, Andre Beyers, ambaye ni mkuu wa masoko wa Airtel Afrika, amesema: "Airtel ni chapa imara katika bara la Asia na inatambuliwa na wateja zaidi ya milioni 190. Utambulisho mpya upo katika nchi 16 za Afrika - Sisi tunategemea kuwa na bidhaa na huduma itakayopendwa zaidi katika Afrika katika kipindi cha miaka minne ijayo. "
Airtel inatarajia kuzindua bidha na huduma mpya kadhaa katika kipindi cha miezi kadha ijayo, kwa lengo la kutoa taarifa muhimu kwa ajili ya wateja wetu ili kuongeza ubora wa maisha yao na kutoa fursa ambayo itawasaidia kuondokana na changamoto zao za kila siku.
Airtel pia imepanua udhamini wake wa MTV Africa Music Awards - ya MAMAs - Tamasha la muziki kubwa kabisa barani Afrika na kutoa na idadi ya bidhaa za kipekee, ikiwa ni pamoja na sauti, picha na mambo muhimu kwa ajili ya MAMAs, kupitia mtandao wake wa ‘Airtel Live’.
0 comments:
Post a Comment