Social Icons

Saturday, November 20, 2010

WASTARA AZAWADIWA MKOKO NA FAMILIA YAKE!

“Kamata funguo hii mdogo wangu, nimekupa zawadi kwa kuwa mshindi wa shindano la Queen of Bongo Film”, Naima akimwambia Wastara (kulia).

HAYAWI hayawi sasa yamekuwa, lile shindano lililokuwa likiendeshwa na gazeti la RISASI kutoka Global Publishers juzi kati lilifikia kikomo na muigizaji wa filamu nchini, Wastara Juma kuibuka mshindi na kujinyakulia zawadi ya televisheni ya kisasa aina ya Samsung yenye inchi 22. Katika mlolongo wa furaha kwa mwigizaji huyo, familia yake pia imemkabidhi zawadi ya gari aina ya Nissan Civilian lenye thamani ya sh. milioni 32. Sherehe ya kukabidhi gari hilo ilifanyika jana Novemba 18 wilayani Bagamoyo katika ufukwe wa bahari uliopo katika Hoteli ya Msalabani.


Familia nzima ya Wastara ikiwa katika picha ya pamoja. Wa kwanza kushoto ni Mariam Juma, Naima Juma, Issa Juma, Wastara Juma, Aisha Juma na Mohammed Juma.

Wastara akipita kwenye zulia jekundu alilotayarishiwa wakati akiingia ukumbi wa sherehe.

Ndugu na mashemeji zake Wastara ‘wakigonga menu’.

Wastara akimlisha Keki dada yake, Naima Juma.

Akimlisha keki mwandishi Shakoor Jongo.

“Dah! Bonge la keki!” ndivyo anaonekana kusema mwandishi wa mtandao huu, Shakoor Jongo, baada ya kulishwa keki ya sherehe.

“Kula keki mume wangu,” Wastara akimlisha keki mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’.


Waoooooooo!! imefunguka

Dada yake Wastara, Naima Juma, akionyesha funguo ya gari kabla hajamkabidhi mdogo wake.

Ahsante dada nakuhaidi nitaitunza gari

Sajuki (kulia) akimshukuru Naima kwa kumzawadia mdogo wake gari.

Wastara akiweka pozi kwenye gari alilopewa

Wastara akiwa ndani ya gari lake akipanga jinsi ya kwenda kupiga breki ya kwanza Songea, ukweni kwake.

0 comments: