Social Icons

Saturday, November 20, 2010

WASHIRIKI BSS WAMWAGA CHOZI TENA

Majaji wa shindano hilo wakifuatilia kwa makini baadhi ya matukio.

WASHIRIKI wa kinyang’anyiro cha Bongo Stars Search (BSS) 2010, kinachorushwa hewani kupitia Runinga ya ITV usiku wa kuamkia leo wamejikuta wakimwaga machozi tena baaada ya wenzao kuondolewa kwenye mchakato huo.

Ishu hiyo iliyoshuhudiwa na paparazzi wetu ilifanyika ndani ya ukumbi wa Water Front, jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki watatu waliweza kuyaaga mashindano hayo.


Haji Ramadhan mwenye namba ya ushiriki (BSS 15), akipata mlo wa usiku muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani, mbele ni Mariam Mohamed (BSS 12).


Baadhi ya washiriki wakilia kwa machungu baada ya majina ya waliouaga mpambano huo kutajwa.


Mtangazaji wa kipindi hicho, Godwin Gondwe, akitaja majina ya washiriki walioingia kumi bora.


Mpiga picha wa kipindi hicho akiwa bize kukabili matukio hayo.


Bella Kombo (kushoto), akinyamazishwa na Winfrida Richard mara baada ya wenzao “kuchapa lapa”.


Baadhi ya watazamaji wakifuatilia kwa makini zoezi hilo.

0 comments: