Ndugu zangu,
Nilipita Dodoma siku mbili kabla ya JK kuhutubia Bunge. Nilizisikia,
fununu za uwezekano wa kutokea kwa tukio lile.
Juzi limetokea, Wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge,
mbele ya Rais wa nchi, mbele ya wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa,
Mabalozi na wengineo. Si habari mpya sana, ilitarajiwa, kwa jinsi
mambo yanavyokwenda sasa. Tutayaona mengi mengine.
Baada ya tukio lile nilitarajia Rais angesonga mbele na hotuba yake
bila kugusia jambo lile. Hilo la mwisho lingewasumbua sana CHADEMA.
Hapana, Rais akagusia tendo lile. Katika nchi, Rais ni mmoja, lakini,
kazi ya Urais ni ya wengi. Najiuliza, je, wasaidizi wake hawajua kabla
kwamba lililotokea lingeweza kutokea ? Kama walilijua, basi,
wangemsaidia Mkuu wa Nchi na kama hawakulijua, nalo ni tatizo.
Nani mshindi?Katika siasa, lililotokea Dodoma ni sehemu ya mapambano ya kisiasa
katika mfumo wa vyama vingi. Chama tawala hakina sababu ya kuogopa.
Kianze sasa kuyazoea mazingira haya mapya. Tunachokiona ni mchezo wa
kisiasa ambao, kama mechi ya mpira, unahitaji team work na wachezaji
mahiri katika kufanikisha ushindi. Maana, tukio lile, kwa wakati huu,
limeliongezea ponti kadhaa za kisiasa CHADEMA.
Watanzania wamelifuatilia, Jumuiya ya Kimataifa imelifuatilia. Ajenda
ya haja ya uwepo wa Katiba Mpya imeharakishwa kufikishwa kwa umma
katika kasi ambayo haikufikiriwa. Watu wanajadili. Ni ajenda ya umma
kwa sasa, CCM wakibaki nyuma, CHADEMA wataonekana kwa umma ndio wenye
dhamira ya kweli ya kuwasaidia.
Naam. Katika dakika hizi za mchezo huu wa kisiasa, CCM imerudishwa
nyuma kwenye lango lake, wanajihami. Na kuna wanaojiuliza nani
mshindi? Mchezo bado unaendelea, tusubiri tuone!
Maggid
Arusha,
Novemba 20, 2010

0 comments:
Post a Comment