Social Icons

Monday, November 22, 2010

TAMASHA LA FILAMU KUZINDULIWA FEBRUARI


TAMASHA la filamu la Mwalimu Nyerere linalojulikana kama Mwalimu Nyerere Film Festival linatarajiwa kufanyika Februari 14,2011 katika Viwanja vya Leaders Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo, litakwenda sambamba na matukio ya utoaji wa tuzo zinazojulikana kama People’s Choice Awards pamoja uzinduzi rasmi wa Shirikisho la filamu nchini ambalo litakwenda kwa jina la (TAFF).
Akizungumza na GPL Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Simon Mwakifamba (pichani kulia), alisema kuwa lengo la kuanzisha kwake ni kuboresha na kuikuza zaidi tasnia ya filamu nchini.
Mwakifamba alisemna kuwa, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya uzinduzi tamasha litaendelea kwa wadau na wageni waalikwa kuangalia filamu zitakazoonyeshwa katika viwanja hivyo.
Februari 15, 2011 huku tamasha likiendelea kutakuwa kukitolewa semina itakayohusu Uandishi bora wa mswada na umuhimu wa haki shiriki na haki miliki kwa msanii.
Februari 16, warsha itaendelea ambapo wadau wa filamu watapatiwa mafunzo ya Ukimwi, uongozi na maadili kwa viongozi wa vikundi vya sanaa.
Februari 17, warsha itatolewa kuhusu Masoko Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na mbinu bora za uigizaji na uongozaji, tarehe 18 itakuwa ni mwisho wa warsha hiyo mafunzo yatakayotolewa ni uongozi bora katika tasnia ya filamu na siku ya mwisho ambayo ni Februari 19, itakuwa ni siku ya utoaji wa tuzo za People’s Choice Awards kwa mshindi kati ya zile nafasi tatu ya filamu zitakazoingia sehemu ya mwisho.
Mgeni anayetarajiwa kutoa zawadi kwa washindi ni mama Maria Nyerere, vile vile kutakuwa na tuzo maalum kwa ajili ya waasisi wa Taifa hili na waliowahi kushiriki katika tasnia ya filamu hapa nchini kama Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na kwa Hayati Rashid Mfaume Kawawa ambaye inasemekana ni moja kati ya Waongozaji wa filamu wa kwanza hapa nchini.
Shirikisho limeomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kudhamini tamasha hili kubwa na la aina yake kwani hadi sasa mdhamini aliyejitokeza ni mmoja tu ambaye ni Focus Media ya jijini Dar es Salaam, gharama zinazohitajika ni fedha za Kitanzania shilingi milioni mia tatu na themanini kwa ajili kuendesha shughuli nzima ya tamasha hili.

0 comments: