Baadhi ya watoto wa Temeke waliyohuzulia Bonanza hilo wakishindana kucheza staili ya Kiduku.
BONANZA la vyuo mbalimbani vya Dar es Salaam lilifanyika jana katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe Temeke jijini Dar es Salaam, ambako kulikuwa na michozo ya aina mbalimbali huku Vyuo kadhaa vikiibuka washindi katika tamasha hilo.
Akiongea na Mateja20, Mratibu wa Bonanza hilo Innocent Melleck, alisema kuwa wameaamua kuandaa Bonaza hilo wakiwa na lengo la kuwakutanisha wasomi wote wa vyuo vya hapa Dar, ili waweze kuhamasisha kwa pamoja suala zima la michezo nchini.
Mratibu wa Tamasha hilo Innocent Melleck akifafanua jambo.
Baadhi ya wanavyuo wakishindana kuvuta kamba ambapo Chuo cha Ustawi wa Jamii kiliibuka mshindi.
shindano la kukimbiza kuku.
Mshindi wa Shindano la kufukuza kuku Taisaly Shaban (katikati mwenye Kaoshi), kutoka katika Chuo cha RCT akiwa amemshikilia kuku wake muda mfupi baada ya kumkamata, wengine kulia na kushoto ni waendesha shughuli hiyo.
Wanaume Family nao walikuwepo.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria viwanjani hapo wakishangilia kwa furaha michezo iliyokuwa ukiendelea kiwanjani hapo.
Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa hewani kupitia kituo cha East Africa Television, Dulla a.k.a mjukuu wa Mbua (kushoto), akiwa kwenye pozi na Dogo Hamidu.
0 comments:
Post a Comment