Social Icons

Thursday, November 18, 2010

MIZENGO PINDA ALA KIAPO!!

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kushoto), akiapishwa mapema leo katika jengo la Ikulu ndogo ya Tanzania Chamwino Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia), akimpa mkono wa pongezi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, muda mfupi baada ya kula kiapo. Dk.Jakaya Kikwete (wa pili kutoka kushoto), akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Msitaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), wengine nyuma ni Mawaziri wa kuu wastaafu, wakiwa na Waziri wa sasa Mizengo Pinda, na wakwanza (kushoto) ni makamu wa Rais Dk.Ghalib Bilal.Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakibadirishana mawazo mara baada ya zoezi la Waziri mkuu kuapishwa.

0 comments: