
Akiongea na Mateja20, mapema leo CBH, alisema kwamba Track hizo ambazo zimeingia juzi katika stesheni mbalimbali za Redio nchini huku zikifanya vizuri katika Club kadha wa kadha jijini Dar, zimerekodiwa katika studio mbili tofauti ikiwemo AM Records na Sharobaro, Chini ya Producer Manecky na Bob Junior a.k.a Mr Choclate Fleva.
Nyimbo hizo zinakwenda kwa majina ya I am inlove, Broda na Oweooh.
Pia CBH alidokeza kwamba kabla ya mwezi huu kuisha atahakikisha anaachia video moja ya wimbo wa I am inlove.
CBH ambae anafanya kazi chini ya Kampuni ya Show Biz Defined Entertaiment (SBD ENT), ambayo inaliteka kwa kasi soko la utengenezaji video Bongo, iliyochini ya meneja wake Eryne D Epidu.
Pia CBH anafanya kazi zake kwa usaidizi mkubwa wa Producer Manecky kijana aliyetoa Hit songs nyingi mwaka huu.
CBH ni msanii ambae amewashangaza wengi kimuziki na upangiliaji wa mavazi, amesema neno music linamaana kubwa sana kwake ikiwa ni pamoja na outlook ya mtu na ndiyo maana kwa amelazimika kua na Designer wawili ambao ndiyo wanao mpangia mavazi yake ya kila siku nao ni JAY CONTENER na AMA.
CBH alimaliza kwa kummwagia shukrani za dhati Sponser wake Emmanuel Mabula, na wananchi kwa kumpokea kwa moyo wote.
3 comments:
CBH ni noumaaaaaaaaaaaaaa
huyo jamaa anatisha sana. Ni mnaigeria?
nimeamini
Post a Comment