Social Icons

Tuesday, November 16, 2010

MHE.JK KIKWETE AMTEUWA TENA MIZENGO PINDA KUWA WAZIRI MKUU

RAIS Jakaya Kikwete, amemteua tena Mizengo Peter Pinda (kulia) kuwa Waziri Mkuu katika awamu ya pili ya uongozi wake. Dk Jakaya, amewasilisha rasmi jina la pinda mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linaendelea na kikao hicho hivi sasa mjini Dodoma. Hivi sasa wabunge wanaanza kumpigia kura Mh. pinda ili kumthibitisha rasmi. Pinda ni Mbunge wa kuchaguliwa kutoka Jimbo la Katavi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kutokana na historia yake safi ya utendaji kazi, wake bilashaka Wabunge wamempitisha kuwa Waziri Mkuu kwa miaka mitano ijayo.

1 comments:

Anonymous said...

Oya! mbona maneno ya hii yanaonekana kwa taabu sana kama vp lekebisha tuone jinsi ilivyokuwa