Social Icons

Wednesday, November 17, 2010

CHEKI HARAKATI ZA KAMERA YA MATEJA20 KATIKA MATUKIO

Mrembo anakwenda kwa jina la Snura Mushi, hapa yuko kwenye pozi kali baada ya kamera yetu kumnasa nyumbani kwake, Mwananyamala Komakoma jijini Dar es Salaam juzikati.
Msanii wa filamu nchini Zamda Salim (kulia), akiwa kwenye picha ya pamoja na Paparazzi wa Global Publishers, Zungu Fedha (katikati) na kushoto ni Salima.
Khaled Chuma 'Chokoraa' (katikati), akiwa kwenye pozi na Pedeshee Bitus Nyema (kushoto), kulia ni rafiki yao ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Wanengua wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta wakitetea ugali wao.

USIKU wa kuamkia leo Mateja20 ilitembelea katika Ukumbi wa Club Sun Cirro pale Sinza jijini Dar es Salaam, na kubahatika kuangalia shoo ya Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani',. Mateja20, haikuishia jukwaani pia ilizama katika chumba ambacho hutumika kupumzika wanenguaji hao mara washukapo stejini, Ambapo ilipenyeza kamera yake na kunasa matukio mbalimbali ya wanenguaji hao, Bila shaka shuka chini zaidi ujionee mambo yalivyokuwa huko nyuma ya jukwaa usiku huo.
Miss Bagamoyo namba tano Pamera John, akiwa karibu na mrango wa kuingilia katika chumba cha kupumzikia wanamuziki, ndani ya Club Sun Cirro.
Mmoja wa wanenguaji wa Twanga Pepeta Regina, akiumwagia moyo wake maji baridi.
Mandera a.k.a Sura Mbaya, akimnong'oneza jambo Regina.
Regina akimsogeza kichwa Mandera baada ya kukolezwa na neno alilokuwa akimwambia.
Mandera akimnong'oneza kwa mara nyingine Regina baada ya kumuomba.
Baada ya maneno hayo bibie Regina hoi...
Regina alipokolezwa... na Mandera akatoka mbio huku Regina akiomba arudi kumpa ... tena.
Queen Suzy akiwa ... back steji.
Queen Suzy akijaribu kuonyesha viji mambo vyake zaidi.
Queen Suzy, baada ya kushtukia kamera alijikuta akidata kama hivi baaanaaa!!!!!
Baada ya muda 'kiduchu' alijisahau na kuendelea kuwapa ... Super K (kushoto), na Said.
Ottilia a.k.a Kandoro (kulia) , akionekana kulegea kiaina kwa Suzy.
Queen Suzy, akiwa amemshika mkono kiunoni Baby Tall, huku akimnong'oneza jambo.
Baby Tall, aliyesimama akiwa kweye pozi na Suzy.
Suzy akifafanua jambo kwa wenzake.

3 comments:

John Arusha hapa. said...

Duh! kumbe wanenguaji hao huwa wana mambo ya ajabu kiasi hicho? asante sana mateja kwa kutufungua macho tunasamini kazi yako endelea kutudondoshea vitu kama hivyo nasi tutakusapoti.

Anonymous said...

Ebwana eeh mateja20 nimeipenda hyo wngu kama vp npatie namba ya Suzy nicheki nae maana huwa namzimia kichizi me Sawe wa Chalinze.

Anonymous said...

Ebwana mateja mdau wako hapa kutoka UK lete picha za sabrina yule wa twanga mwambie kuna mshikaji kakuzimika hapa,tuwekee picha zake tumuone.