Wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika Mashariki kwa mara nyingine jana walishinda nje ya geti la Mahakama Kuu wakitaka walipwe malipo yao ambapo walisema kuwa hawataondoka katika eneo hilo hadi kieleweke.
Kitendo hicho kilisababisha dola iingilie kati na kuwatawanya wazee hao kutoka katika eneo hilo majira ya saa 1:45 usiku kwa kutumia kikosi maalum cha kutuliza ghasia maarufu kama FFU
Kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu na msemaji wa Mahakama hiyo Mh. Francis Mutungi alisema kuwa kimsingi wazee hao wana haki lakini bado serikali inafanya utaratibu wa kumaliza suala lao.

Msajili wa Mahakama na msememaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mh. Francis Mutungi, akiongea na mwandishi wa habari wa Globla Publisher na runinga ya TBC 1 (hawapo pichani) kuhusu hatima ya wazee hao kulala hapo na kuziba barabara kwa muda wa saa 10.
Kaimu kamanda wa Kanda Maalum, Charles Kenyela akiwasihi wazee hao kutawanyika katika eneo hilo kwa kuwaambia muda uliobakia siyo wa kazi na kuwataka waondoke kwa sababu serikali inashughulikia malalamiko yao.
Mmoja wa wastaafu akiwa amelala katikati ya barabara ya Sokoine huku akisema haondoki hadi kieleweke.
Wazee hawa aliamua kudondosha ibada baada ya muda wa swala kufika wakiwa eneo la tukio.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasi a.k.a FFU wakiwasili eneo la tukio na kuwaomba wazee hao kuondoka ili wasiwadhuru lakini wazee hao hawakutii amri ndipo nguvu ya ziada ikatumika.
Askari wa kutuliza ghasia akishuka katika gari maalum na kwenda kwa Kaimu Kamanda Kanda Maalum, Charles Kenyela kwa ajili ya kupata maelekezo ya jinsi ya kuwatawanya wazee hao kwa kumwaga maji ya kuwasha.
Kaimu Kamanda akiongea na waandishi baada ya zoezi la kuwatawanya wazee hao kukamilika majira ya saa 1:45 usiku na kusema kuwa kazi imefanyika salama kulingana na maagizo ya mamlaka husika.
Huyu ni mbwa wa polisi mwenye cheo cha Koplo akiwa ndani ya gari maalum la polisi tayari kwa kukabiliana na jambo lolote atakapotakiwa kufanya hivyo.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakishuka katika gari lao kwa ajili ya kutimiza lile waliloagizwa na uongozi wa juu wa jeshi hilo.

0 comments:
Post a Comment