Social Icons

Monday, October 18, 2010

WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU WATUA NCHINI


Mwenyekiti wa waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Kabinga Pande (kulia) akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa siasa, waandishi wa habari na waangalizi wa uchaguzi kutoka SADC juu ya ujio wa ujumbe wa waangalizi hao na majukumu yao wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 31 mwezi huu leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa watanzania kudumisha amani na kuonyesha ukomavu wa kisiasa uliopo nchini hasa kabla na baada ya uchaguzi.
Viongozi wa waangalizi wa uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) waliokaa, Dkt Tomaz Salomao ambaye ni katibu mtendaji kutoka Botswana (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa waangalizi hao kutoka SADC, pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Kabinga Pande (katikati) wakitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo watakayoyafanya katika kipindi chote cha uangalizi wao hapa nchini kwa Mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa waangalizi wa SADC leo jijini Dar es salaam.

Washiriki wa mkutano wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka nchi za SADC wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa

MWANAFUNZI CHUO AVUTA MSHIKO WA SUPER PESA!!


Huku droo ya Supa Pesa ikiendelea kutoa mamilioni kwa washindi wake kupitia bahati nasibu inayochezeshwa nchini kote, wikiendi iliyopita imemkuta mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma,tawi la Mwanza, Catherine Nyamoni, akibahatika kujinyakulia kiasi cha milioni moja fedha taslimu.Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 23, alisema,’ Kweli mimi nilikuwa kati ya watu ambao sitilii maanani michezo ya bahati nasibu wala kuwahi kushiriki kati shindano lolote maishani mwangu. Lakini wiki chache zilizopita nilipokuwa nasikiliza redio nyumbani, nilipata nafasi ya kumsikiliza mshindi wa milioni kumi akipigiwa simu kujulishwa kuhusu ushindi wake.

Basi pale ndipo nilipata hamasa kubwa na kuamua kutopitwa na nafasi ya kujaribu bahati yangu. Nilishiriki kwa kutuma ujumbe mfupi kama walivyoelekeza na baada ya kujaribu mara kadhaa nimepata ushindi. Namshukuru Mungu nimefanikiwa na kupata ushindi.’Catherine aliongezea kusema, ‘ Nitatumia hela za ushindi kuendeleza masomo yangu kwa kununua kompyuta itakayonisaidia kufanya kazi chuoni kwa ustadi zaidi na vilevile hela itakayobaki ninatarajia kutumia kama mtaji wa kuanzisha biashara ndogo ili kujipatia kipato cha kila siku.Kushiriki droo ya Supa Pesa ni rahisi, inahitaji kutuma ujumbe mfupi wenye neno SUPA kwenda namba 15777. Hii inakuwezesha wewe kuingia moja kwa moja kwenye ushindani wa shilingi milioni moja kila sikui na ukishiriki kutuma Ujumbe mfupi wa simu zaidi ya mara nne basi utakuwa kati ya washindani wa milioni kumi kila wiki.

UTAPELI WA WENZETU WA WEST AFRICA.!

Angalieni huu Utapeli wa West Africa.!

Mr.DIYA MUSA
BANK OF AFRICA(B.O.A)
OUAGADOUGOU BURKINA-FASO
WEST AFRICA


Dear Friend,

I know that this message will come to you as a surprise. I AM A SECRETARY OF FOREIGN REMITTANCE DIRECTOR BOA BANK HERE IN OUAGADOUGOU BURKINA FASO. I Hope that you will not expose or betray this trust and confident that i am about to repose on you for the mutual benefit of our both families.
I need your urgent assistance in transferring the sum of ($7.6)million to your account within 14 banking days. This money has been dormant for years in our Bank without claim. I want the bank to release the money to you as the nearest person to our deceased customer, the owner of the account died along with his supposed next of kin in an air crash since July 31st 2000.
I don't want the money to go into our Bank treasurer as an abandoned fund. So this is the reason why i contacted you so that the bank can release the money to you as the next of kin to the deceased customer. Please I would like you to keep this proposal as a top secret and delete it if you are not interested.
Upon receipt of your reply , i will give you full details on how the business will be executed and also note that you will have 40% of the above mentioned sum if you agree to handle this business with me.
Best Regard.
Mr.DIYA MUS

KCB yakisaidia kitengo cha ‘sickle cell’ Muhimbilili

Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akimkabidhi Mkuu wa huduma za maabara wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Emmael Moshi hundi ya milioni 10/- zilizotolewa na benki hiyo leo kama msaada kwa kitengo kinachohudumia wagonjwa hao ili kusaidia uimarishaji wa maabara ya kituo hicho iweze kuhudumia wagonjwa wengi zaidi. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Christina Manyeye.

Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie (kulia) akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa milioni 10/- kwa kitengo kinachohudumia wagonjwa wenye ‘sickle cell’ cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo ili kusaidia uimarishaji wa maabara ya kituo hicho iweze kuhudumia wagonjwa wengi zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Christina Manyeye.

Mkuu wa huduma za maabara wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Emmael Moshi (kulia) akizungumzia athari za ugonjwa wa ‘sickle cell’ wakati wa hafla ya KCB Tanzania kukabidhi msaada wa milioni 10/- kwa kitengo kinachohudumia wagonjwa hao leo ili kusaidia uimarishaji wa maabara ya kituo hicho iweze kuhudumia wagonjwa wengi zaidi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Joram Kiarie.

China na tanzania zatiliana saini mkataba wa ujenzi lst leo jijini dar


Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Oliver Mhaiki (kulia) wakitiliana saini mkataba wa ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ujenzi ya BCEG ya China Bw. Jia Jianhui mara baada ya kutiliana saini mkataba huo jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Oktoba 18, 2010). Katikati ni Afisa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Benas Mayogu.picha kwa hisani ya Mohammed Mhina.

PICHA: MICHUZI JR BLOG

0 comments: