Social Icons

Wednesday, October 20, 2010

KAMPUNI YA KITANZANIA YAFANYA MAAJABU AFRIKA!!!

Afisa Mtendaji wa SYSCORP Media (kushoto) akiwaonesha wasimamizi hao mchakato wa mipango ya kampuni yake kwenye komputa ndogo (Laptop). Kulia ni Alex Cudaback, kushoto Michael Schleidt ambao ni wasimamizi.
KAMPUNI ya SYSCORP Media ya nchini leo imetembelewa na wasimamizi wa kimataifa wa makampuni ya wajasiriamali barani Afrika baada ya kufanikiwa kuingia kwenye 15 bora ya mashindano yaliyoshirikisha makampuni 2,700 ya barani Afrika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa SYSCORP Media, Beatus Kaboja, aliupokea ugeni huo kutoka Marekani na Australia na kuwapa siri ya mafanikio yake.
Baada ya kampuni hiyo kuingia kwenye 15 bora fainali za kupata tatu bora na mshindi wa kwanza zitafanyika Nairobi nchini Kenya, Desemba 6 mwaka huu ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha dola za Kimarekani laki moja.


Kaboja akiwafafanulia jambo wasimamizi hao.


Alex (kulia) akiomba ufafanuzi zaidi kutoka kwa Kaboja (hayupo pichani).


Kaboja (kushoto) akiwaonesha wasimamizi hao mtambo unaotumiwa na kampuni yake kutengeneza mabango ya barabarani ambayo ni moja ya shughuli za kampuni yake. Wengine ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.


……Akiwaonesha baadhi ya mabango yaliyotengezwa na kampuni yake.


Wasimamizi wakiangalia vyuma vilivyoandaliwa kwa ajili ya kuweka matangazo makubwa ya barabarani.


Mmoja wa wasimamizi akiwahoji wafanyakazi wa kampuni hiyo kuhusu suala la mapato.


0 comments: