Social Icons

Thursday, October 14, 2010

UTABIRI WA BABA WA TAIFA UMETIMIA


TAIFA la Tanzania leo linatimiza miaka kumi na moja toka kifo cha mwasisi wake, Baba wa Taifa, hayati Julius Kambarage Nyerere kilichotokea katika hospitali ya Mtakatifu Thomas, jijini London, Uingereza.
Kwa Watanzania walio wengi, leo ni siku muhimu zaidi kwani wakati wakikumbuka kifo hicho, bado siku kumi na saba tu kufikia Uchaguzi Mkuu ambao utafanyika nchini kote Oktoba 31, 2010.
Vyombo mbalimbambali vya habari vimekuwa vikiandika au kukumbushia hotuba za Baba wa Taifa kama mwongozo na dira katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Baadhi ya hotuba hizo ni pamoja na zile zinazoelekeza Watanzania ni kiongozi gani bora wa kumchagua siku ya kupiga kura.
Lakini katika moja ya hotuba hizo ipo aliyowahi kuitoa kwenye mkutano wa Umoja wa Vijana wa CCM, mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi unaingia.
Mwalimu alisema serikali imekubali kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa, lakini wasiwasi wake ni kuwa, haamini kama watapatikana viongozi ambao watakuwa tayari kupokea matokeo na kwamba, watakuwa si wa kukimbilia mahakamani baada ya kushindwa.

Alizungumzia mengi, likiwemo la kupata viongozi bora, wanaojali wapiga kura wao na pia wale watakaodumisha Muungano wa Visiwani na Bara.

Karibu maneno mengi kwenye hotuba zinazorushwa hewani na vyombo vya habari vya kielektroniki yametimia na ndiyo mambo yanayozua gumzo katika jamii kwa sasa.

0 comments: