FILAMU ya Unsung Heroines inayohusu historia na maisha ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro inatajwa kuwa mojawapo itakayofanya vizuri katika tamasha la filamu la EFF linalotarajiwa kuanza leo kwenye ukumbi wa New World Cinema jijini Dar es Salaam.
Ubora wa filamu hiyo ya Dr. Rose Migiro ambaye amesomea taaluma ya sheria inaonyesha mwanzo wa maisha yake, tangu alipozaliwa miaka 50 iliyopita katika bonde la Mlima wa Kilimanjaro, baadaye kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na kisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa tamasha hilo lililozinduliwa Jumanne iliyopita katika hoteli ya Coral beach, Tayana Tabenda alisema kwamba hii ni moja ya filamu ambazo mashabiki wa tasnia hii hawatakiwi kuikosa kabisa, pia tamasha hilo kila wikiendi litafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.

0 comments:
Post a Comment