Social Icons

Tuesday, October 12, 2010

TIGO YAZINDUA HUDUMA YA MALIPO YA KABLA

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo, leo imezindua huduma mpya ya mtandao ya malipo ya kabla inayojulikana kama Tigo Pre-Paid Blackberry.

Huduma hiyo imezinduliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Patric J. Makungu katika hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam.


Mtandao huo, kwa mujibu wa Tigo, unatumika katika simu za aina ya Blackberry na laini za Tigo tu.

Dk Makungu amesema kuwa hayo ni matokeo mazuri ya utekelezaji wa sera za serikali ambazo kwa ujumla wake zinalenga kuweka mazingira mazuri ya ushindani na ubunifu katika sekta binafsi ambayo wananchi wanashuhudia kupitia uboreshwaji wa huduma na kupungua kwa gharama za huduma zinazotolewa.

Aidha amesema kuwa viwangio vya chini vilivyowekwa na kampuni ya Tigo katika vifurushi vya huduma hii ya Blackberry ni ushuhuda wa jinsi kampuni ya Tigo ilivyojipanga na kutumia fursa hiyo vizuri.

Kwa upande wake Ofisa Mwendeshaji Biashara Mkuu, Diego Gutierrez, alisema mtandao huo una kasi kubwa kwa mawasiliano na kwamba wateja wake watafurahia huduma hiyo.

Guitierrez alisisitiza kwamba huduma hiyo itakuwa na gharama ndogo ambayo itawawezesha wateja kuwasiliana kwa barua-pepe, kuwasiliana kuhusu hafla mbalimbali na kuwasiliana katika maongezi binafasi, na kadhalika.


Mshereheshaji wa shughuli hiyo, Denis Busulwa ‘Ssebo’, akiwajibika.

Meneja Uboreshaji wa Tigo, David Zacharia, akielekeza namna ya kuunganisha huduma hiyo.


Mgeni rasmi wa shughuli hiyo Dk. Patrick J. Makungu, akifungua hafla hiyo.


Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwajibika katika shughuli hiyo.


Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakielekezana jambo muda mfupi kabla ya shughuli hiyo kuanza.

Dk. Makungu (kushoto), akijadiliana jambo na baadhi ya viongozi wa Tigo. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, kulia ni Meneja Uboreshaji na Uendeshaji wa Tigo, David Zacharia.


Diego Gutierrez akimkabidhi zawadi ya simu aina ya Blackberry mmoja wa waandishi wa kujitegemea aliyeshinda kwenye mchezo wa kubahatisha uliochezeshwa hapo.



Afisa Biashara Msaidizi wa Tigo, Tawonga Mpore, akimkabidhi simu mmoja wa walioshinda mchezo wa kubahatisha.

Zacharia, akichukua chakula muda mfupi baada ya kumalizika kwa zoezi zima la uzinduzi wa huduma hiyo.

Baadhi ya vyakula vilivyokuwa vimeandaliwa katika hafla hiyo.

0 comments: