Jackson Mmbando (kulia) akimkabidhi funguo za gari, Hamad Mohamed, baada ya kujishindia.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, leo imemkabidhi gari jipya aina ya Suzuki (Vitara Grand) mteja wake, Hamad Mohamed, baada ya kujishindia mchezo wa kubahatisha wa “Sajili na Ushinde” katika bonanza la kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere lililofanyika viwanja vya Tanganyika International School jijini Dar es Salaam.
Katika makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando, alisema kuanzia kesho wateja wa kampuni hiyo ambao hawajasajili ‘line’ zao hawataweza kupiga simu isipokuwa wataweza kupokea tu na baada ya siku 30 hawataweza kupiga wala kupokea mpaka watakapozisajili.

Meneja Mauzo wa Tigo mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Nkya (kulia), akimkabidhi pikipiki, Humphrey Shao, baada ya kujishindia mchezo huo.
Meneja Masoko na Matangazo wa Tigo, Redemptus Masanja (kulia), akimkabidhi pikipiki, Sauda Abdalah, baada ya kushinda mchezo huo.
Msanii wa vichekesho Dickson Makwaya a.k.a Bambo akijiandaa kwa ajili ya kusakata kabumbu kwenye bonanza hilo lililofanyika viwanja vya Tanganyika International School jijini.
Wanenguaji wa Bendi ya Diamond Musica wakiwa kazini kwenye bonanza hilo.
Bambo (kulia) akitoana jasho na mmoja wa mashabiki waliohudhuria bonanza hilo.
Wasanii wa kundi la vichekesho la East Africa TV, wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment